Na Saleh Ally
TUMEKUBALIANA mara zote kwamba tuseme ukweli kila inapohitajika kufanya hivyo kwa ajili ya maendeleo ya mpira wetu, ni jambo zuri.
Hata hivyo, hii haitupi nafasi ya kusemasema ili mradi, kulalamika bila ya sababu ya msingi au kushutumu na kushambulia taasisi fulani au watu bila ya kutulia na kuwazua mambo kwanza.
Hapa nawazungumzia wale baadhi ya mashabiki wa Yanga waliofanya vurugu kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Yanga ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Mbeya City.
Ukiangalia mwamuzi, hakika alijitahidi sana, aliifanya kazi yake vizuri hata kama ni makosa yalikuwa madogo sana ya kibinadamu. Angalia bao la Yanga, kwa mwamuzi asiye makini ni vigumu sana kuona halikuwa bao au la. Lakini unaona mwamuzi huyo kaifanya kazi yake vizuri, utata unabaki kwetu lakini uhalisia, lile ni bao.
Rudi kwenye tukio lililosababisha penalti, hakuna ubishi beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustapha yuko ndani ya eneo la 18 na ameshika ule mpira, haina mjadala na mwamuzi kaifanya kazi yake kwa kufuata sheria 17 za soka.
Hapa ndipo unapaswa kuanza kujiuliza, wale wanaolalamika kipi hasa wanachokilalamikia na ukiwakuta wengi wao wanazungumzia kwamba Deus Kaseke aliangushwa na beki wa Mbeya City wakati wakikimbia, inawezekana waligongana na mwamuzi msaidizi hakuonyesha kweli kama kuna faulo.
Mwamuzi huyo msaidizi ndiye alionyesha kuwa mpira umefunga msitari na Yanga ikaandika bao, sasa vipi ionekane kawaonea pale? Kuna mengi sana ya kujiuliza.
Ajabu zaidi wakati haya yanatokea ambayo inaonyesha wazi kuwa mechi hiyo haikuwa na makosa ya mwamuzi kufanya watu wapandwe jazba hivyo. Maana kama ni jazba, hata Mbeya City nao wangeweza kufanya hivyo kwa kisingizio cha mpira haukuwa umevuka msitari.
Lawama zinaelekezwa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), tena wengine wakiwadhihaki viongozi wao kwa sababu zisizokuwa na msingi, si sahihi.
Hakuna sababu hata kidogo ya kusema maneno ya kashfa kwa viongozi wa taasisi hizo kwa kuwa si kweli wao kuwa pale ndio imepitishwa watukanwe au dhihaka ya kila aina.
Si saw ahata kidogo watu kuamini kila upungufu sababu kuu itakuwa ni imetokana na TFF au TPLB. Jiulize, vipi mashabiki hao hawazungumzii kuhusiana na kiwango cha kikosi chao na kuangalia wachezaji wao walifanya kipi kilichokuwa sahihi kuipigania timu yao? Kiwango walichokionyesha dhidi ya Mbeya City ni sahihi kweli, ni kile ambacho kinaweza kuonyesha Yanga ilionewa?
Yanga ilipiga mashuti mangapi yaliyolenga lango ndani ya dakika 90? Sote tunajua hata matano hayafiki na mengi si mashuti sumbufu! Nafasi walizotengeneza ni ngapi na walizitumiaje? Tunajua kuhusiana na ukweli lakini baadhi wanajaribu kutaka kuonyesha wameumizwa na hili nimelisema mara nyingi sana, zile tabia za kutaka kuwaonyesha wengine kwamba wewe ni shabiki kindakindaki na umeumia sana. Soka ni starehe yako, furahia na umia kivyako si lazima uweke matangazo, haina msaada wowote.
Kikosi cha Yanga hakikuonyesha soka safi, soka la kuitisha Mbeya City na kuiweka katika wakati mgumu kiasi cha kusema walilazimika kubebwa na mwamuzi.
Inapendeza sana kama mashabiki wakawa wanatafakari vitu kabla ya kuanza kuvifanyia kazi, pia wajiondoe katika ile hali ya kutaka kila jambo lazima kuwe na vurugu au matusi.
Watu wasiojielewa pekee ndio wanaweza kujivunia uwezo wa wa kutukana au kufanya vurugu. Anzeni kumhoji Kocha Kaze kutokana na aina ya uchezaji, kikosi chake kwa maana ya ushambulizi, idadi ya mabao ya kufunga na kadhalika. Wapeni maswali wachezaji wenu, waambieni waongeze juhudi waipambanie timu, wanachofanya sasa, bado!
Wadau wote wakemee hii tabia ya kujifanya kila timu insposhindwa kutimiza majukumu uwanjani lawama tff, tplb, waamuzi ma wakati mwingine anasingiziwa simba. Waangalie tomu yao inachezaje. Kama na kocha nar ameongia kwenye hizi politics ni jambo la aibu mno, aangalie profesheno yake. Mambo mengine atuachie siso mashabiki uchwara tusiojua abc za soka zaidi ya unazi tuu.
ReplyDeleteWaambie Manyani hao waache mambo ya kizamani
ReplyDeleteHujawahi ikosoa simba ndio shida ya mchambuzi kupenda timu yake nyie nisimba tambeni mulijipa kuongoza ligi kabla hamjacheza vipolo vyenu wachambuzi munapoteza mvuto kama marefaree wetu wanaishia tanzania tu jitathimini
ReplyDeleteHapana shaka kwa asiye kufahamu Bw. Saleh Ally. Kila shabiki anaifaham chuki yko dhidi ya Yanga sc toka ulipokosa Uofisa Habar kipindi cha Manji
ReplyDeleteAiseee
Deletemimi ni shabiki wa yanga na pia ni shabiki wa soka la tz kwakweli mpk sasa sijajua timu yetu tunalalamikia kitu gani beki wetu ni kweli alinawa sasa pale sijui refa angefanya nini labda sijajua vizuri malalamiko yapo kwenye nini eti pale??ifike muda tuimize timu yetu wanachezea sana nafasi za wazi golini
ReplyDeleteMakuma nyie mnaounga mkono waaamzi wa Tanzania bila kujiuliza mbona hakuna mwamzi hata mmoja anaenda kuchezesha CHAN? Usimba na uyanga unawaponza makuma tu
ReplyDeleteMama yako pia alikuleta duniani kupitia hicho kiungo
DeleteNafikiri hatakuja kucoment tena,,,akiludi bac bangi imehucka
Deletekuma wewe na mama yako mzazi mbwa wewe mkosa adabu wewe tupo kwaajir ya mpira matusi ya nini ndiyo tatizo mama zenu wakibakwa harafu mkazaliwa watu kama nyinyi
DeleteShida ni kwamba Yanga mwaka huu wanautafuta ubingwa kwa nguvu zote wakishindwa kucheza mpira basi wanageuka kuwa mabondia imekuwa timu yenye kulalamika kusikoisha na fujo nyingi kama vile ni timu ya ndondo cup wanadhani kila mechi wao ndo wenye haki ya kushinda tu
ReplyDeleteHata Simba nao wanautafuta ubingwa kwa nguvu. Wakilegea tu ubibgwa unakwenda kwingine. Ila nimefaham Saleh kakosa hoja za mashiko za kuwalaumu Yanga kwa lawama zao kwa mwamuzi. Ukisema kuhusu shorts on target na off targets kuwa Yanga walipiga chache, sasa hicho ni kigezo cha wao kutolalamika dhidi ya penalt ya wazi walionyimwa? Waandishi wengi wanaharibiwa na ushabiki wa timu zao; na Saleh kajipambanua dhahiri yeye ni mshabiki wa Mikia. All in all, mapambano ya Yanga katika harakat za kusaka ubingwa zinaendelea na Inshaa Allah, Yanga atatwaa ubingwa japo mizengwe ni mingi kwake
DeleteKuna baadhi ya washabiki wa Yanga ukiambiwa akili zako zinafanana pigana ,hv Kuna timu imebebwa Kama Yanga round ya Kwanza wamesahau mechi na gwambina Holi halali refa kalikataa,mechi na Kagera Sugar penalti ya wazi wamenyimwa Kagera mbona hamkusema marefa,eti mizengwe ni mingi kwa Yanga these people are very stupid,Yani nyie ndo mpewe penalti,magoli ya timu pinzani yakataliwe ikitokea kwenu ata Kama si tukio la kweli mnawasingizia marefa hakuna timu ya Mpira hapo utopolo ni kikundi Cha Siasa kilichojificha nyuma ya pazia la football
DeleteHata ww hujakatazwa kusema unachokiwaza. Hata kikiwa kikundi cha wapiga dege waliojificha katika soka, ww kinakupunguzia kitu gani? Waache walaumu hata ww unaruhusiwa kulaumu. After all, lawama zitolewazo haziwez kubadili matokeo ya maamuzi
Deletematako weeee
ReplyDeleteAcha matusi. Hapo ndio unapopoteza maana ya utu wako. Utamtukanaje mama yako? Huna adabu wewe hata kama umekasirika
ReplyDeleteHuyu anayetukana nadhan hajitambui na hajui kuwa kumtukana mtu ni kujitukana mwenyewe na wazazi wake pia. Mungu Amsamehe maana hajui atendalo
ReplyDeletekwahyo unavomaanisha goli walilofunga yanga sio goli, why udhan kaseke aligongana na beki wkt uwezo wa ww kuiangalia tena mechi unao? wamekuruhusu vp umiliki blog ya habari kwa ujinga huu unaotaka kuwaaminisha mbumbumb
ReplyDeleteBwana Salehe Ally unaukumbuka ushindi wa Simba dhidi ya Mbeya city mara ya mwisho ulipatikanaje? Msituone wajinga hasira zinakuja kwasababu.
ReplyDeleteSeleh ni shabiki wa Simba na anashindwa kujificha hata katika kivuli cha fimbo. Nadhan matokeo ya droo ya Yanga yamemfurahisha sana bila kujali Yanga kaonewa katika tukio la wazi kabisa. Sijajua faida ya yeye kubeza lawama za wanajangwani.
DeleteKwa hiyo akiizinisha goli hutakiwi kuizinisha penati hata kama ni kweli penati?kaseke kaangushwa ndani ya kumi na nana haikuhitaji kwenda kwa mganga kuagua kuwa penati kwa sababu yeye ndiye alikuwa na faida na ule mpira,leaf katafuna filimbi.hamuliongelei hilo,na ndiyo wanalolalamikia watu waache watu na hisia zao
ReplyDeleteTutawapiga tu wakileta ujinga tena sana
ReplyDeleteKwa mechi ile refa hakuwa na tatzo kabsa,,,tatzo ni cc mashabiki tunaamini kuna timu za kushinda na kuna timu za kufungwa bila hata kujali uwezo wa wachezaji wetu kwenye mechi husika cku hyo wameamkaje
ReplyDeleteVyura mtakoma mwaka huu.mtajinyonga kwa uchungu
ReplyDeleteMpira wa bongo Mungu asimamie tu, wahandishi wanazi mashabiki wachochezi kila kona inavutia kwake,ila nataka nimuombe kocha kuhusu kupanga kikosi juzi carihno kwani alikuwa nje, yucuba je kwanini nawakati walisafili na timu wkt walikuwa fiti hii mechi tulikuwa tunamaliza dakika90 tu haya mengine yasingekuwepo ila atukati tamaa tutafika tu
ReplyDeleteYanga yetu bado timu mbovu . Tujipange tu kuliko kusingizia mikia wanabebwa.
ReplyDeleteyule beki alimzidi kaseke kwa mbele ndio maana sio penat,na wote waliteleza mpaka chini.
ReplyDeleteHakuna shirikisho hapo uchafu mtupu
ReplyDelete