CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaamini kesho atapata pointi tatu muhimu mbele ya wapinzani wao Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.
Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwana nafasi ya kwanza na wana pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.
Mbeya City haijawa na mwendo mzuri kwa msimu wa 2020/21 ambapo imecheza jumla ya mechi 18 imekusanya jumla ya pointi 14.
Kaze amesema kuwa anatambua wapinzani wao wataingia ndani ya Uwanja kusaka pointi tatu hilo halimpi shida kwa kuwa wamefanya maandalizi mazuri.
"Tuna wachezaji wazuri ambao wapo ndani ya kikosi imani yetu ule ushindani ambao upo nasi tutapambana kuendelea kusaka ushindi ndani ya uwanja hakuna tunachohofia.
"Kila mmoja anajua tunahitaji pointi tatu nao pia tunajua kwamba wanahitaji pointi tatu hivyo ni suala la muda kusubiri itakuaje, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Miongoni mwa watengeneza mipango ambao walikuwa nje ya uwanja kwa muda ni Carlos Carinhos ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha tayari ameanza mazoezi na ana pasi mbili za mabao na amefunga mabao mawili kati ya 29 ya Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment