March 16, 2021

 


KLABU ya Al Ahly ya Misri leo Machi 16 imesepa na pointi tatu muhimu ikiwa ugenini kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika,  hatua ya makundi.

Uwanja wa Des Martyrs ubao ulisoma AS Vita 0-3 Al Ahly ambapo mabao yalianza kupachikwa kupitia kwa Mohamed Sherif dakika ya 6.

Dakika ya 19 Mohamed Magdy yeye alipachika bao la pili dakika ya 19 na kufanya waende mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0.

Ni Taher Mohamed alipachika bao la tatu na la mwisho dakika ya 78.

Kundi A kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika limekuwa na ushindani mkubwa ambapo kinara ni Simba mwenye pointi 10 huku Al Ahly akiwa na pointi 7 nafasi ya pili.

Al Merrikh ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi moja na AS Vita ipo nafasi ya tatu na ina pointi 4.


5 COMMENTS:

  1. Vita club imeshikilia ticket ya simba kwenda robo final na tasmini fupi ya mchezo wa vita na Alahly ni kwamba yawezekana kabisa vita walitumia nguvu kubwa katika mechi yao ya Kwanza kule misri na kukosa wakati sahihi wa kurecover. Na yawezekana kabisa kuwa Juma shabani ni vita club na vita club ni juma shabani akikamatwa yeye timu imekamatwa pia. Kitu kingine kibaya zaidi vita waliwakosea heshima Ahaly kwa kucheza an open game.Ahly bado ni timu kubwa Africa ingawa mpira wa Afica una Mambo mengi nyuma ya pazia vita sio timu nyepesi hivyo kukubali kipigo Cha paka mwizi. Ila kama Kuna timu za Africa zimeathirica na vibe la kukosekana kwa Mashabiki uwanjani basi timu za Congo, isipokuwa zimebakiza mentality ile ile ya upambanaji ugenini na Simba kuanzia leo waanze kazi ya kuichimba vita.

    ReplyDelete
  2. Simba sport club is on good position to qualify quarter final since one point is needed only to make a total of 11points which can not be there reached by any club in their group except national al ahaly of Cairo .

    ReplyDelete
  3. Simba they have advantage of one game in Dar es salaam, they can just choose the key plyers from Vita and ask they to take Covid 19 tests, then chess them away, like what they did with Almerekh, ahahahaa.
    FYi that is African ⚽...

    ReplyDelete
  4. Kila la kheri chama kubwa simba sc katika mashindano yanayowahusu mabingwa tu!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic