WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Klabu ya Simba leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni Luis Miquissone alianza kupachika bao la kuongoza kipindi cha kwanza dakika ya 17 na bao la pili lilipachikwa na Mohamed Hussein dakika ya 38.
Chini ya Didier Gomes ambaye ni kocha mkuu akisaidiana na Seleman Matola walikwenda mapumziko ubao ukisoma Simba 2-0 Al Merrikh.
Kipindi cha pili Simba ilipachika bao la tatu kupitia kwa Chris Mugalu dakika ya 49 na kuwafanya Simba kuwapa mzigo mzito wapinzani wao ndani ya Uwanja wa Mkapa.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 10 ikiwa nafasi ya kwanza huku Al Merrikh ikibaki na pointi moja nafasi ya nne.
Ulikuwa ni ushindi wa kimyakimya kwa sababu mashabiki walipigwa pini mazima na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuipa sapoti timu yao.
Licha ya mashabiki kutokuwepo kwenye uwanjani bado wachezaji walipambana kusaka matokeo na kuibuka na ushindi wakiwa nyumbani.
Pongezi kwa Aishi Manula na safu yake ya ushambuliaji kwa kulinda lango la Simba ndani ya dakika 90.
Tadeo Lwanga alikuwa ni mtibua mipango akishirikiana na Joash Onyango ambaye hakuweza kumaliza dakika 90 kwa kuwa aligongwa na mpira kichwani kwenye harakati za kuokoa hatari.
vipi hamjui kuwa Simba imeingia robo fainali? au mmeamua potezea
ReplyDeleteBado mdau, tunahitaji point moja zaidi ili tujihajikishie
DeleteWale vizabina zabina wa Utopolo wamejificha wapi?
ReplyDeleteWachezaji 8 wana corona? Dhuu
DeleteYa platnum yamejirudia
DeleteMwambieni kilo 800 aunganishe na kesi Morrison Cas
DeleteCongo waliwabakiza wachezaji 6 kwa kudai wana Corona.Ulisikia Simba wakipiga kelele au kulalama ?
ReplyDeleteVipi kesho kuna Press Conference ya Morrison??
Lro amecheza na kutoa assist!
Silent killer, kama alivotamka Mheshimiwa Manara
ReplyDelete