March 12, 2021

 

MSHAMBULIAJI wa timu taifa ya Tanzania na klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco, Saimon Msuva amesema kuwa anaamini klabu za Namungo na Simba zina nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kama tu watapambana.

Namungo juzi Jumatano walipoteza mchezo wao wa kwanza wa kundi D la michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, kutoka kwa Raja Casablanca ya nchini Morroco, huku Simba wao wakiwa wanaongoza kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia nafasi Namungo kwenye michuano hiyo Msuva amesema: “Nimekuwa niwafuatilia kwa ukaribu mkubwa wawakilishi wa Tanzania Kimataifa, Simba  na Namungo kwa upande wangu naamini timu hizi zitafanya vizuri endapo tu zitapambana mwanzo mpaka mwisho.

“Namungo wanatakiwa wasijione kuwa ni wageni wakashindwa kufanya vizuri, mpira ni ule ule muhimu ni kupambana kwani wana wachezaji wazuri ambao wanaweza kuipa mafanikio timu hiyo, pia niwapongeze kwa hatua ambayo wamefikia,"

2 COMMENTS:

  1. Kila ki2 kitakuwa kama unavoxema

    ReplyDelete
  2. Msuva ni msaada na ni moja ya faida kubwa ya wachezaji wetu kutoka kucheza nje amekuwa exposed kwenye shughuli za wakubwa uzuri ni kwamba Msuva ameonesha mapema umuhimu wake kwa kutumia uzoefu wake kuzisaidia timu za nyumbani pia, hongera sana . Niliona jinsi alivyokuwa akiwatia ndimu Namungo kabla ya mechi yao na Raja casa Blanca ya Morocco kwa kiasi fulani Msuva ndie aliekuwa man of the match wa Namungo behind the scene ama nyuma ya pazia Hadi kuwapa wakati mgumu Raja kwao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic