March 14, 2021


 MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Bongo, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa anaona wazi kwamba kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos hawezi kucheza ndani ya kikosi hicho kutokana na kasi ya Ligi Kuu Bara.

Carlinhos, raia wa Angola ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho ambacho kipo chini ya Kaimu Kocha, Juma Mwambusi baada ya Cedric Kaze kufutwa kazi, Machi 7.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya ambapo imeweka wazi kwamba imepata zaidi ya CV 72.

Kashasha amesema:-”Naona kwamba bado Carlinhos hajawa na ile nguvu ya kucheza ndani ya Yanga kwa sababu mpira ule wa kugonganagongana ndani ya uwanja anaonekana hauwezi, yaani ni aina ya wachezaji ambao hawataki shida jambo ambalo halipo kwenye ligi yetu," .

Ndani ya ligi Muangola huyo amecheza jumla ya mechi sita na amehusika kwenye jumla ya mabao matatu na ana pasi mbili za mabao kati ya 36 yalifungwa na timu hiyo.

5 COMMENTS:

  1. Hilo nililisema mapema watu wakanizodoa sana. Ukweli huyu hawezi ligi hii, anaweza kuwa anajua mpira ila hana fiziki ya kupambana

    ReplyDelete
  2. Ataishia kusaka mademu wa bongo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Moira sio tu nguvu za kupambana na kusukumana.Mbona amefunga na kuwa na assists NYINGI zaidi ya wanaojua kupambana akina Junior Lukosa na wakina Nchimbi?

      Delete
  3. Junior Lokosa amecheza ligi?Nchimbi inajulikana Yanga walimchukua basda ys kuwapiga hattrick walipocheza na Polisi msimu uliopita.Jamaa ana kilo 40 utacheza vipi mpira wa nguvu unaochezwa kwenye ligi ya Tanzania.Ndio maana alitupa kijingumi dhidi ya Kengold.
    Hata kumfungia ni kumuonea tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic