MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa tatizo kubwa linaloitesa Klabu ya Yanga kwa wachezaji wake kushindwa kufanya vizuri ni makosa ya ufuatiliaji wa wachezaji.
Kashasha amesema kuwa ikiwa watu watafuatilia kwa umakini aina ya wachezaji ambao wanaletwa ndani ya kikosi hicho kwa mbwembwe, wengi hawana hadhi ya kucheza ndani ya kikosi hicho jambo ambalo linafanya wawe na mwendo wa kusuasua.
Kutokana na mwendo wa kusuasua kwenye mzunguko wa pili chini ya Cedric Kaze raia wa Burundi pamoja na mzawa Nizar Khalfan ambaye alikuwa ni msaidizi walifutwa kazi Machi 7, uongozi wa Yanga uliamua kufuta benchi hilo la ufundi.
Alex Kashasha amesema:-" Makosa ambayo yanaigharimu Klabu ya Yanga ni moja yule anayefanya scouting ndani ya Yanga anafanya ujanjaujanja mwingi kwa kuleta wachezaji ambao hawana hadhi ya kucheza ndani ya Yanga.
"Kwa mfano mchezaji kama Yikpe (Gnamien), aliwahi kuja Yanga na ubora wake haukuwa mkubwa akaondoka pia hakuwa na sifa za kucheza katika kikosi hicho.
"Mwingine ni David Molinga naye alikuja kwa mapambio mengi na hakuweza kufanya vizuri mwisho wa siku naye pia akaondoka.
"Kwa sasa kuna Saido Ntibanzokiza huyu ana unafuu ila ni majeruhi hapo unaona bado tatizo pia hata umri unaonekana kwamba umekwenda.
"Yacouba, (Sogne) huyu naye pia ni mgonjwa hivyo unaona kwamba bado kuna kazi kubwa ndani ya scouting ya Yanga.
"Mshambuliaji mwingine ni Michael Sarpong bado amekuwa anakimbiakimbia tu na zaidi ya mechi 21 ambazo amecheza ana mabao manne.
"Hivyo ni muhimu kwa Yanga kuweza kuangalia namna bora ya kufanya scouting ili kupata wachezaji ambao watakuwa na hadhi ya kucheza kwenye timu hiyo ikiwa wanahitaji mafanikio," amesema.
Ni ukweli huo ila mwalimu kashasha utawakera ukisema hivyo.
ReplyDeletebinafsi hanikeri kwakuwa nafahamu vema uwezo wa mwalimu kashasha katika kuchambua....katika hili hachambui kwa kubeza bali anaongea fact na kwa kujenga.....kwanza kashasha mwenyewe ni mwana yanga halisi,namfahamu kwa kuwa nimeshasafiri nae kwenda nchi kadhaa katika mechi za kimtaifa za yanga na timu ya taifa.
DeleteWacha wapewe vidonge wapone, hii club ishakuwa jipu Tanzania
ReplyDeletesasa mbona uto waliwapokea kama vile wafalme...walilala uwanja wa ndege wanawasubiri!
ReplyDeletePovu ruksa
ReplyDeleteBaada ya kuwachambuwa wachezaji wa Yanga sasa tunakuombea uwachambuwe wa Mnyama
ReplyDeletekina lokasa ya mbongo
DeleteUnajua kashasha namuheshimu sana lkn kusema wachezaji wanaokuja yanga hawana uwezo wa kuchezea yanga huyo sarpong alikua Ryon sport ya Rwanda inashiriki ligi kuu kama ilivyo yanga Yacuba naye katokea Kotoko nayo inashiriki ligi kuu km ilivyo yanga mchezaji kuperform timu moja ni kitu kingine na kwenye timu ni kitu kingine kwahiyo yanga wasajili wachezaji kutoka wapi ndio wawe na hadhi ya kucheza yanga sasa yanga wanauwezo wakusajili wachezaji kutoka alhaly au mamelod kwahiyo wachezaji waliokua wanasajiliwa mwanzo wakati wanachukua makombe walikua wanawatoa wapi mbinguni? Km msimu huu usajili kasimamia mwenye hela yake GSM km kaingia chaka mwenyewe ndio kaliwa ata ulaya hivi vitu vipo
ReplyDeleteWakati wanashinda mechi za mzunguuko was kwanza mbona chambuzi hizo hazitokea acheni unafki
ReplyDelete