March 12, 2021


 RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Wallace Karia amethibitisha kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea Ujumbe wa Baraza la FIFA kuwakilisha nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza.


Taarifa rasmi ambayo imetolewa leo na TFF imeelezza kuwa Karia ameamua kujiondoa kwenye mchakato huo ambapo alikuwa anawania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Shirikisho la FIFA.

Karia amesema:-“Ni kweli, nafasi za kuingia kutoka Afrika zinagombewa kutokana na uzungumzwaji wa lugha, sisi tulikuwa tunagombea nafasi za kuingia kwa lugha ya Kiingereza [Anglophone].

“Kutokana na makubaliano ya juu, mgombea pekee wa Urais wa CAF Patrice Motsepe tayari anatoka Anglophone (maana yake anaingia moja kwa moja kwenye baraza wajumbe wa FIFA) kwa hiyo inabaki nafasi moja, wagombea tulikuwa sita, katika hao sita mmoja anatoka kwenye ukanda wetu (CECAFA).

“Jana tulikuwa na kikao chetu cha CECAFA tukakubaliana kwa sababu mimi ni kiongozi wa zone tukakubaliana kumwachia mwenzangu wa Kenya Nick Mwendwa.”


Uchaguzi wa CAF unatarajiwa kufanyika leo jijini Rabat, Morocco.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic