KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa, anaamini kurejea kwa baadhi ya nyota wake muhimu waliokuwa na majeraha kutaisaidia timu hiyo kufanya vizuri na kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Coastal Union.
Yacouba ambaye hajaichezea Yanga mchezo wowote tangu kuanza kwa mwaka huu kutokana na majeraha ya misuli, tayari amekwisharejea uwanjani na yupo kwenye orodha ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Coastal leo.
Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri ya
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, katika mchezo wa mzunguko wa
kwanza uliopigwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Oktoba 3, mwaka
jana.
Akizungumzia kurejea kwa nyota hao, kocha Kaze amesema: “Kwanza siwezi kusema kama tulikuwa tunapata wakati mgumu kusaka matokeo, bali ni changamoto za kiufundi na kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wetu muhimu.
“Lakini jambo zuri ni kwamba tayari baadhi ya nyota hao muhimu ikiwemo Yacouba wamerejea, hali hii inanipa matumaini makubwa ya kuamini tutafanya vizuri katika michezo yetu ijayo.
“Tunataka kuanza na mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Coastal Union, ambao ni lazima tushinde ili kuendelea kujiimarisha katika uongozi wa ligi,”
Yanga inakamatia usukani wa ligi na pointi zao 49
walizokusanya, baada ya kucheza michezo 21 wakishinda mechi 14 na kutoa sare
michezo saba.
Tulijua itafika siku Yanga itafungwa!uko wapi ule wimbo wa eti ndiyo timu pekee haijafungwa! Saleh jembe kama vile walijua kitakachotokea wakaamua potezea mechi
ReplyDeleteKwa mpira wa leo Yanga inaanza kupotea. Unbeaten kwishaaaaaaa
ReplyDeleteKwa ss itabaki kuitwa kinara wa ligi Ila Mnyama akirudi kuchukua nafasi yake watahamia kwenye bingwa wa kihistoria
ReplyDeleteKocha wa uto anza kufunga mizigo yako vzr maana huna muda mrefu japo kwa gem ya leo wachezaji ndo wamekuangusha
ReplyDeleteWatu wa Tanga wabaya sana mtu na mdogo wake wote wamemgonga mtu mmoja. Daaaahhhh!!!! ni noma sana
ReplyDeleteWasimtafute mchawi. Wamejiroga wenyewe hao
ReplyDeleteJambo jema kwa Utopolo ni kuwa pamoja na kuwa tayari wamekwisha ukosa ubingwa msimu huu, lakini watashiriki ligi ya mabingwa Africa kwa mgongo wa Mnyama
ReplyDeleteChania shati yule, piga huyu, zomea yule. Tunaonewa shitaki FIFA, Fukuza ma kocha timua, mwisho wa siku haya ndio matokeo
ReplyDeleteTimu yangu inakwenda chini miguu juu lakini bado hatujakata tamaa na ndio mana leo kocha kawapa hongera wachezaji wake kwa namna walivopambana. Timu nzima ilikuwa imepwaya kama isiyokuwa na nguvu ijapokuwa Mr Senzo ali jitahidi toka mwanzo Mpaka mwisho kutokana na mapenzi yake kwa timu yake yasiyo na mipaka
ReplyDeleteSENZO YUPO KAZINI, HAKUNA MAPENZI BILA PESA
Delete