STAA wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya Kings Music Records, Alikiba amesema kuwa hatarudi tena kucheza Ligi Kuu Bara kama ambavyo alifanya akiwa na Coastal Union msimu wa 2018-19.
Alikiba alisema alicheza Coastal kwa sababu alikuwa anahitaji kwenye Biography (wasifu) yake kuonyesha kuwa aliwahi kucheza soka la ushindani kwa levo ya ligi kuu na anashukuru kuwa alifanikiwa kufanya hivyo.
Kiba amesema kwa sasa atakuwa anacheza soka kwa ngazi za mtaani kwa kuwa anapenda sana mpira wa miguu na ana kipaji kikubwa, lakini suala la kurudi tena ligi kuu haliwezi kutokea na atabaki anakomaa na muziki.
“Mimi ni mwanamuziki na nitabaki huku kwa sasa, watu wasitarajie kuniona tena ligi kuu, nilicheza Coastal kwa sababu nilikuwa nahitaji kuipa thamani zaidi Biography yangu angalau ionekane kuwa niliwahi kucheza ligi kuu,” amesema Kiba.
Kiba kwa sasa ni nahodha wa timu ya Bin Slum FC ambayo inashiriki Ramadhan Cup inayofanyika katika Viwanja vya JK Park.
0 COMMENTS:
Post a Comment