April 20, 2021


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, 
amempa kazi ya ukalimani kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Haruna Niyonzima kwa kuwasiliana na winga Tuisila Kisinda raia DR Congo ambaye hajui lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Mwambusi ambaye kwa sasa ni kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, amekuwa akimtumia kiungo huyo kufikisha maelekezo yake kwa winga huyo ili kuweza kufuata anachotaka kocha huyo.


Niyonzima alifanya kazi hiyo katika mchezo wa Jumamosi uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United.


Championi ambalo lilikuwepo uwanjani hapo lilimshuhudia, Niyonzima akiinuka kwenye benchi kwenda kumtafasiria Kisinda kila alipokuwa ameitwa na kocha huyo kupokea maelekezo yake kwa kuwa anatumia lugha ya kifaransa na Kilingala pekee.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo, Niyonzima amekuwa akitumika kumfikishia maagizo winga huyo kutokana na kutumia Kilingala na Kifaransa ambayo anaitumia pia Niyonzima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic