BAO la pili alipachika dakika ya 86 ndani ya 18 na kufikisha jumla ya mabao 10 wakati Azam FC ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ni Prince Dube aliyeanza kupachika bao la kwanza dakika ya 8 kwa mkwaju wa penalti baada ya kiungo Mudhathir Yahya kuchezewa faulo ndani ya 18.
Licha ya kipa namba moja wa Azam FC, Mathias Kigonya kumpisha kipa namba mbili Wilbol baada ya kuumia bado ilikuwa ngumu kwa Mtibwa Sugar kupenya mbele ya Azam FC.
Ushindi wa leo Aprili 9 unaifanya Azam FC kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 pale walipokutana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Azam FC inafikisha pointi 47 baada ya kucheza mechi 25 ipo nafasi ya pili huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 50.
Mtibwa ngoja wakajipange ligi daraja la kwanza kama wataweza kurudi tena
ReplyDelete