April 9, 2021

 




FT: Al Ahly 1-0 Simba
Wawakilishi wa Tanzania,  Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika leo wanapoteza mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Licha ya kichapo hicho ina tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali na ina pointi 13 huku Al Ahly ikiwa nafasi ya pili na pointi 11.
Zinaongezwa dakika 90
Dakika ya 90 Manula anaokoa
Dakika ya 89, Zimbwe anatoka anaingia Dilunga
Dakika ya 81 Nyoni anatoka anaingia Mugalu
Dakika ya 75 Chama anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Al Ahly 
Dakika ya 73 kona wanapata Simba
Dakika ya 72 Kapombe anachezewa faulo 
Dakika ya 68, Wawa anafanya jaribio linakwenda nje ya lango na Kagere anafanya jaribio linaokolewa na mlinda mlango
Dakika ya 67, Kahata anachezewa faulo nje kidogo ya 18
Dakika ya 65 Luis anacheza faulo akiwa eneo la Al Ahly 
Dakika ya 65, Kahata anacheza faulo
Dakika ya 64 Luis anaokoa na Kahata anachezewa faulo 
Dakika ya 63 Nyoni, Kapombe, Wawa, Manula
Dakika ya 61 Al Ahly wanapeleka mashambulizi kwa Manula
Dakika ya 59 Ahly wanaanza na kipa wao
Dakika ya 57, Kagere anafanyiwa faulo inapigwa na Zimbwe
Dakika ya 56 Manula anaanzisha mashambulizi 
Dakika ya 53 Mzamiru anaingia anatoka Mkude 
Dakika ya 50, Kapombe anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika ya 47 Chama anapoteza mpira
Dakika ya 45, Francis Kahata anaingia kuchukua nafasi ya Bwalya
Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika

 Kipindi cha pili 

Al Ahly 1-0 Simba

Mapumziko 

Zinaongezwa dakika 2

Dakika ya 45 Kapombe anapeleka mashambulizi Al Ahly

Dakika ya 43 Junior wa Al Ahly anapewa huduma ya Kwanza na kutolewa akiwa Kwenye machela

Dakika ya 40, Clatous Chama anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Al Ahly 

Dakika ya 39 Luis anatengeneza pasi ndefu kumfuata Kagere anaichelewa 

Dakika ya 38, Luis anachezewa faulo

Dakika ya 34 Jonas Mkude anachezewa faulo 

Dakika ya 33 Zimbwe anamwaga maji lango la Al Ahly inaokolewa 

Dakika ya 31, Goal Sharif

Dakika ya 29 Kagere anatengeneza nafasi ila haileti matunda

Dakika ya 27 Manula anaokoa hatari ndani ya 18 inakuwa Kona haileti matunda 

Dakika ya 26 Kapombe anafanya jaribio linaokolewa

Dakika ya 25 Al Ahly wanalifuata lango la Manula

Dakika ya 23 Ahmed Ramadhan anafanya jaribio zuri akiwa nje ya 18 linapaa 

Dakika ya 22 Kagere anacheza faulo

Dakika ya 21 Mohamed Sharif anafanya jaribio zuri ndani ya 18 baada ya mabeki wa Simba kushindwa kuokoa hatari ila inakwenda nje 

Dakika ya 17, Luis anaingia Kwenye mtego wa kuotea

Dakika ya 16 Onyango anaokoa ndani ya 18, Al Ahly wanapata kona ya Kwanza 

Dakika ya 15 Chama anatoa mpira nje

Dakika ya 14 Kagere anachezewa faulo

Dakika ya 13 Kagere anaotea

Dakika ya 12, Mohamed Sharif anafanya jaribio kwa Simba linapaa juu ya lango la Manula

Dakika ya 11, Chama anapiga faulo Simba wanakosa nafasi 

Dakika ya 9, Luis anachezewa faulo nje kidogo ya 18 anapewa huduma ya kwanza

Dakika ya 7, Manula anaokoa hatari

Dakika ya 4 Manula anaokoa hatari na kumuanzisha mashambulizi kwenda Al Ahly 

Dakika ya 3 Kagere anachezewa faulo

Dakika ya 2 Chama anapoteza mpira


Dakika ya 1 Manula anaokoa

Meddie Kagere leo ameanza kikosi cha Kwanza akichukua nafasi ya Mugalu ambaye alikuwa alianza mechi zilizopita

7 COMMENTS:

  1. Hongera mtani mmecheza kwa kujiamini sana

    ReplyDelete
  2. Msimu 2019 Mnyama wa Uchebe kama sikosei alipocheza na Al Ahli kwao, alichapwa tano bila na kwa Vita nne moja, natumuone Mnyama wa 2021 chini ya Mfaransa na kijana Konde Boy. Kwa Simba huyu wa msimu huu aliyelishwa akashiba, atayejaribu kumzuwia ajuwe kaazirika vibaya na amekwisha

    ReplyDelete
  3. Hapo SIMBA mlipofika, ndio MWISHO WENU. Get la nusu fainal limefungwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie ndio mnaozimiaga viwanjani Yani katika timu jumi na sita Simba ndio timu Bora alafu Chura mmoja anakuja eti Apo ndo mwisho kweli nchi hii WEHU wengi

      Delete
  4. Hapo tulipofika ni pakubwa sana hapajafikiwa na timu yeyote Afrika ya Mashariki na wanaoionea hasadi Simba na kukosa uzalendo kutumia kwa chuki wamechelewa na katu hawatifika popote

    ReplyDelete
  5. Heri ujinga wa kuuza kuliko ubaradhuli wa kununua. Utopolo walianza dua hii tokea tunacheza na Plateau mpaka sasa. Kila siku dua zinafeli jwa sababu ni husda tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic