IMEELEZWA kuwa baada ya mabosi wa Simba kumalizana na manahodha wao kwa kuwaongezea mikataba mipya sasa ni zamu ya beki wa pembeni Shomari Kapombe.
Nahodha Mkuu, John Bocco mwenye mabao 10 ndani ya ligi msimu huu pamoja na nahodha msaidizi Mohamed Hussein mwenye mabao mawili ndani ya ligi jana Aprili 28 walitambulishwa rasmi na Simba kwamba wameongeza mikataba yao.
Baada ya nyota hao kuongeza inaelezwa kwamba tayari wamekamilisha mazungumzo na Kapombe ambaye naye mkataba wake unafika ukingoni.
"Simba wanajambo lao kwa sasa hawapo tayari kuwaacha wachezaji ambao wapo kwenye mpango wao. Unaona kwamba tayari Mohamed na Bocco wameshatambulishwa na kuoneshwa kwa mashabiki basi kuna wengine wanafuata ikiwa ni pamoja na Kapombe.
"Kapombe naye mkataba wake unaisha msimu utakapokamilika hivyo mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote naye atasaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia timu hiyo.
"Orodha ni ndefu kwani wachezaji wengi mikataba yao kwa sasa inafika ukingoni, hata Mkude, (Jonas) naye kandarasi yake ipo ukingoni, Mzamiru, (Yassin) ni suala la kusubiri," ilieleza taarifa hiyo.
Mohamed alikuwa anatajwa kuingia rada za timu za Afrika Kusini pamoja na Bongo ambapo watani zao wa jadi Yanga walikuwa wanatajwa kuwania saini yake.
Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes aliweka wazi kwamba hatakubali kuona mchezaji anayemhitaji akiondoka ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kikiwa kimetinga hatua ya robo fainali.
Hakuna nyota yeyote wa Simba aliyekuwa na akili yake timamu akakubali kujiunga na yanga
ReplyDeleteHa haaaa
Delete