April 29, 2021


LICHA ya mshambuliaji wa JKT Tanzania, Danny Lyanga mwenye mabao 9 kuanza kuchochea mvua ya mabao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana dhidi ya Mbeya City bado mambo yalikuwa magumu kwao na kuweza kubebeshwa zigo la mabao kutoka kwa Mbeya City.

Wakiwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, ubao baada ya dakika 90 ulisoma Mbeya City 6-1 JKT Tanzania jambo lililowafanya Wajeda hao kuacha pointi tatu mazima Mbeya.

Ni Lyanga wa JKT Tanzania alifungua pazia la mabao hayo ambapo ilikuwa ni dakika ya 8, bao hilo lilidumu kwa muda wa dakika 10 kwani dakika ya 19 Mbeya City walianza kufanya yao kwa kuweka usawa kupitia kwa Kibu Denis.

Dakika ya 45+1David Mwasa alipachika bao la pili na kuwafanya waende mapumziko ubao ukisoma Mbeya City 2-1 JKT Tanzania.

Kipindi cha pili Mbeya City waliandika bao la tatu dakika ya 49 kupitia kwa Richardson Ngondya na bao la nne lilipachikwa na Juma Luizio dakika ya 68 na alifunga la tano dakika ya 88 lile la sita ni mali ya Pastory Atanas dakika ya 90+5.

 Dakika ya 89 ya mchezo mshambuliaji wa JKT Tanzania  Lyanga katika harakati za kupiga faulo mpira wake ulikutana na tumbo la mwamuzi Tatu Malongo ambaye alianguka chini na kupewa huduma ya kwanza.

Hata hivyo aliweza kurejea katika ubora wake na kuendelea kutimiza majukumu yake na kukamilisha dakika 90 Uwanja wa Sokoine na ubao ulikuwa ukisoma Mbeya City 6-1 JKT Tanzania. 

Ushindi huo unaifanya Mbeya City kufikisha pointi 30 ikiwa nafasi ya 13 huku JKT Tanzania ikiwa nafasi ya 17 na pointi 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic