BAADA ya jana Jumatatu kuanza rasmi kambi yao ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), chini ya kocha Boniface Pawasa, kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa soka la ufukweni ‘beach soccer’ kimetamba kujipanga kutumia michuano hiyo kusaka fanya tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia.
Tanzania ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha timu ya Taifa ya Burundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 12-9, katika michezo yao miwili iliyofanyika katika Viwanja vya Fukwe za Coco, Dar es SalaamMachi 30 na Aprili 3, mwaka huu.
Tanzania imefuzu michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo mara baada ya kushiriki michuano iliyopita nchini Misri.
Akizungumzia maandalizi yao, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Deogratius Lucas alisema: “Baada ya kumaliza likizo yetu fupi ya sikukuu za pasaka, kikosi tayari kimeingia kambini kwa ajili ya kuanza rasmi kambi ya kujiandaa na michuano ya AFCON.
“Tunataka kuanza maandalizi
mapema kwani malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ili kusaka
tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa kuwa tunajua timu zitacheza
,”
0 COMMENTS:
Post a Comment