KIUNGO wa zamani wa Simba anayekipiga ndani ya kikosi cha Biashara United, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ amesema kuwa sababu kubwa ya kupoteza mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Yanga ni kukosa umakini ndani ya kikosi chao.
Katika mchezo huo wa Jumamosai Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Yacouba Sogne dakika ya 59 ya mchezo, akiunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na mlinzi wa kushoto wa timu hiyo Adeyum Saleh.
Kipigo hicho ni cha pili mfululizo kwa Biashara tangu kurejea kwa ligi, na licha ya kupoteza michezo miwili mfululizo, Biashara wanaendelewa kusalia katika nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi zao 40 walizokusanya kwenye michezo 26 waliyocheza mpaka sasa.
Akizungumzia mchezo huo, Redondo amesema “Tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga, kwangu ulikuwa mchezo mzuri kwa pande zote mbili, tulicheza kwa nidhamu kubwa kutokana na kufahamu ubora wa wapinzani wetu.
“Tulijua Yanga wangekuwa na presha kubwa ya kutafuta matokeo na ndiyo maana tulikuja na mbinu ya kuzuia na kushambulia kwa pamoja, lakini kwa bahati mbaya tulifanya kosa moja la kupoteza umakini ambalo wapinzani wetu wamelitumia na kufunga bao."
Shida ni viapo vya kutumwa na watu wengine nje ya club
ReplyDelete