April 14, 2021


 ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, amesema kuwa macho yao yote ni kwenye mechi zote ambazo zitachezwa na kuwataka mashabiki pamoja na timu kuzingatia kanuni.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio yasiyo ya kinidhamu ambapo mashabiki wamekuwa wakiwapiga waamuzi kwa machupa na wakati mwingine kuingia uwanjani jambo ambalo haliruhusiwi kikanuni.

Suala hilo limekuwa likisababisha adhabu kwa timu husika pale inapobainika tatizo hilo.

Lala salama kumekuwa na matukio mengi ambayo yanahatarisha usalama kwa wachezaji pamoja na waamuzi jambo ambalo kwa sasa linafuatiliwa kwa ukaribu.

Kasongo amesema:"Mechi zote ambazo zimebaki tunazitolea macho na kuzitazama kwa ukaribu, lengo ni kuona kwamba kila kitu kinakwenda sawa na hakuna kinachoharibika.

"Mashabiki, wachezaji na timu kiujumla ni muhimu kuzingatia kanuni ambazo zipo kwani mpira unaendeshwa na kanuni ambazo zipo," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic