April 23, 2021


JAWAB Sabri kocha mpya wa viungo ndani ya Klabu ya Yanga ambaye ametambulishwa rasmi jana Aprili 22 inaonyesha kwamba ana uzoefu wa kufanya kazi na timu mbalimbali za Afrika.

Raia huyo wa Morocco anauwezo wa kuongea lugha tatu ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kiarabu na Kifaransa jambo ambalo litarahisisha mawasiliano na wachezaji wa kikosi hicho ambacho kinapambana kusaka taji la Ligi Kuu Bara.

Miongoni mwa timu ambazo amefanya nazo kazi ni pamoja na Klabu ya Raja Casablanca ilikuwa ni msimu wa 2019 ambapo aliweza kufanikisha pia timu hiyo kutwaa taji la Morocco.

Pia amewahi kuwa mkuu wa kitengo cha viungo katika kituo cha Royal Moroccan Football Federation ilikuwa ni kuanzia Septemba, 2016- 2019.


4 COMMENTS:

  1. CV nyembamba, sehemu mbili tuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usukurupuke kujibu au kufanya kitu kabla ya kupata muda wa kufikiri,ukiendelea na tabia hiyo utakuwa ukifeli katika kila jambo katika maisha yako.Kwanza haijaelezwa kuwa ni sehemu mbili tu alizofanyia kazi bali hizo mbili ni miongoni mwa timu alizofanyanazo kazi(rudia kusoma hiyo taarifa).
      Pia hata kama zingekuwa ni hizi mbili tu,kinachomata sio utitiri wa sehemu ulizofanyia kazi bali ukubwa wa timu na perfomance yako vitu ambavyo vyote vinambeba;Raja Casablanca si tu ni timu kubwa Morrocco,ni miongoni mwa timu kubwa barani Africa pia,na imeelezwa kuwa katika kipindi chake Raja walichukua ubingwa wa Morocco.
      Hivyo hata kama atatokea mwingine aliyewahi kufundisha timu kumi zenye hadhi ya chini bado CV yake haiwezi kulingana na huyo aliyetoka Raja.

      Delete
  2. Tunaomba CV ya kocha mkuu wa yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic