April 23, 2021

 MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa nyota wao  Mohamed Hussein bado yupoyupo ndani ya Simba kwa sasa na hatokwenda Yanga.



Imekuwa ikielezwa kuwa nahodha huyo msaidizi yupo kwenye rada za Yanga ambayo inahitaji kuboresha kikosi chake.


Mkataba wa Hussein ambaye ni beki mzawa inaelezwa kuwa mkataba wake umebaki muda wa mwezi mmoja kumeguka.

"Tumeskia hizo taarifa za beki ba nahodha wetu kutaka kusajiliwa Yanga, lakini nipende kuwaweka wazi kuwa huyo bado ni mchezaji wetu kwa kuwa ana mkataba na Simba.


"Lakini pia uongozi una matarajio makubwa ya kumpa mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya Klabu yetu,".


Chanzo: Championi

2 COMMENTS:

  1. Duuh mwezi mmoja, sasa mnasubir nini kumsainisha.... Zimbwe yuko vizur mpeni mkataba asije akaondoka

    ReplyDelete
  2. Wacha aende watu wa magazeti ninkawaida yao kutunga story ili mradi kuitetemesha Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic