April 8, 2021


 IMEELEZWA kuwa kipa namba moja wa Klabu ya Azam FC, David Kissu ameambiwa kwamba anapaswa ajifunze namna ya kudaka kwa kipa anayeaminiwa kwa sasa Mathias Kigonya.

Kissu alianza kwa kasi mzunguko wa kwanza na alikuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza jambo ambalo lilipeleka jina lake kuitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Ila ghafla mambo yalikuwa magumu kwake kwa kushindwa kuendelea na kasi ambapo makosa yake ya kufungwa mabao ya nje ya 18 yalikuwa yakimponza na kuigharimu timu.

Baada ya kucheza mechi 7 bila kupoteza pointi tatu, mechi yao ya kwanza kupoteza ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar ambapo Kissu alitunguliwa bao nje ya 18.

Pia wakati Azam FC iliposhinda mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar, beki wa Kagera Sugar, David Luhende alimtungua Kissu nje ya 18 jambo lililowafanya mabosi wa Azam FC kumleta Kigonya.

Habari kutoka ndani ya Azam FC zimeeleza kuwa Kissu ameambiwa kwamba anapaswa ajifunze kudaka upya ikiwa makosa yataendelea anaweza kuchimbishwa jumla.

"Kissu bado yupo Azam FC ila ameambiwa kwamba anapaswa kujifunza kwa kipa mwenzake ambaye anadaka kwa sasa.

"Makosa yakiwa yanajirudia hasa kwa nafasi ya kipa hilo ni kosa ambalo linaigharimu timu hivyo ni muhimu kujifunza ili kuweza kuwa bora zaidi, ikiwa atashindwa basi anaweza kuondoka" ilieleza taarifa hiyo.

Kocha wao wa makipa ni Idd Abubakar ambaye anawanoa vijana hao wanaotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zao za nyumbani.

Mchezo wao ujao wa ligi ni dhidi ya Mtibwa Sugar, unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex Aprili 9, saa 1:00 usiku.

Hivi karibuni, kocha msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati alisema kuwa kazi kubwa ya kipa ni kuzuia lango lisifungwe ikiwa kutakuwa na makosa lazima yafanyiwe kazi.

1 COMMENTS:

  1. Alikuja na makeke mengi anataka kushindana na Manula kumbe pazia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic