BEKI wa kulia wa kikosi cha klabu ya Simba, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’, amefunguka kuwa ana matumaini makubwa kikosi chao kitarejea na moto uleule wa kukusanya pointi tatu muhimu kwenye kila mchezo ili kutetea tena ubingwa wao msimu huu.
Simba Queens ndiyo vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake ambapo mpaka sasa wamekusanya pointi 39 kwenye michezo 15 waliyocheza.
Akizungumzia, Densa amesema: “Kama mabingwa watetezi tumekuwa na mwendelezo mzuri msimu huu katika dhamira yetu ya kutetea ubingwa tulioutwaa msimu uliopita.
“Hivyo nina matumaini makubwa
hata baada ya mapumziko haya ya dharura tuliyopata, kikosi chetu kitarudi na
moto uleule wa kukusanya pointi tatu muhimu kwenye kila mchezo ulio mbele
yetu,”
0 COMMENTS:
Post a Comment