April 14, 2021

 

MLINDA mlango namba moja wa kikosi cha klabu ya Simba, Aishi Manula amekiri kuwa uwepo wa kipa namba mbili wa kikosi chao, Beno Kakolanya ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo zinamfanya azidi kuwa bora.

Manula amekuwa katika kiwango cha hali ya juu katika siku za hivi karibuni ambapo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ameruhusu mabao mawili tu, katika michezo nane aliyosimama langoni, huku katika hatua ya makundi ya michuano hiyo akiwa ameruhusu bao moja pekee katika michezo minne aliyocheza.

Kutokana na rekodi hizo Manula ameonekana kuzivutia timu mbalimbali kutoka nje ya nchi ambazo zinataka kupata huduma yake ikiwemo Al Merrikh ya Sudani, ambayo iliweka wazi kuwa wapo tayari kuweka mezani dau la Shilingi Milioni 230 na mshahara wa Milioni 18 ili kukamilisha usajili huo.

Akizungumzia kiwango chao, Manula amesema: “Nashukuru Mungu kwa uwezo ambao nimekuwa nikionyesha katika siku za hivi karibuni, napokea pongezi nyingi kutoka kwa watu wangu wa karibu lakini binafsi naamini ubora huu si wangu pekeangu, bali wa kila mchezaji ndani ya kikosi chetu.

“Naamini pia uwepo wa makipa wengine wa kikosi hiki kama, Beno na Ally Salim ni miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia mimi kuwa bora zaidi kwa sasa,”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic