April 8, 2021


 MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Azam FC, Prince Dube amebakiza dakika 270 za kukutana na mshikaji wake wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina mkononi ina mechi 10 za kuhitimisha ligi, itakutana na wapinzani wao Yanga baada ya kucheza mechi tatu ambazo ni dakika 270.

Itaanza na Mtibwa Sugar, Aprili 9, itakuwa na kazi mbele ya JKT Tanzania, Aprili 16 kisha itakutana na Dodoma Jiji, Aprili 22 baada ya mechi hizo Dube atakutana na mshikaji wake Mwamnyeto kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Aprili 25, Uwanja wa Mkapa.

Raia huyo wa Zimbabwe anakumbukumbu ya kupata maumivu ya mkono walipokutana na Mwamnyeto kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na kumfanya akae nje kwa muda wa wiki sita akipewa matibabu.

Mchezo huo ulikamilika kwa ubao kusoma Azam FC 0-1 Yanga na bao lilipachikwa na Deus Kaseke hivyo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa sababu Azam itahitaji kulipa kisasi na Yanga nao wanahitaji kulinda rekodi.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo Dube atakuwa na jukumu la kutaka kupenya kwenye ngome ya ulinzi ya Yanga inayoongozwa na Lamine Moro pamoja na Mwamnyeto.

Pia huenda ataongeza umakini katika namna ya ukabaji na kusaka ushindi kwa kuwa anakumbuka kwamba alikaa nje ya uwanja kwa muda akitibu majeraha yake baada ya kugongana na Mwamnyeto.

Aprili 9, Azam FC itakuwa na kazi dhidi ya Mtibwa Sugar na Aprili 10, Yanga itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya KMC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic