BENCHI la ufundi la klabu ya Azam limejipanga kuhakikisha linamsaidia mshambuliaji wao, Prince Dube kuongeza idadi ya mabao anayoweza kufunga kwa kumpa programu maalum kati yake na viungo washambuliaji wa timu hiyo.
Dube ndiye kinara wa ufungaji mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara ambapo amefanikiwa kuweka kambani mabao kumi, akifuatiwa na Meddie Kagere na John Bocco wa Simba ambao wamefunga mabao tisa kila mmoja.
Akizungumzia mpango huo, kocha msaidizi wa Azam, Vivier Bahati alisema: “Kama benchi la ufundi baada ya kufanya tathimini ya michezo yetu iliyopita tumegundua kuwa, mshambuliaji wetu Prince Dube amekuwa akitengeneza nafasi nyingi za kufunga kutokana na mikimbio yake langoni mwa mpinzani.
“Lakini changamoto kubwa inakuwa kwa viungo washambuliaji wanaosimama nyuma yake kumsaidia, ambao kwa bahati mbaya huwa wanashuka sana, hali inayomfanya Dube ashindwe kuwa na msaada kutokana na kubaki pekeyake.
“Hivyo tunalifanyia kazi hilo ili
kuhakikisha kwenye michezo yetu ijayo viungo watakaopangwa nyuma ya Dube,
wanakuwa karibu zaidi naye muda mwingi ili kumuongezea nafasi ya kufunga mabao
mengi zaidi,”
0 COMMENTS:
Post a Comment