April 18, 2021


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa licha ya kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kutoka kile ambacho kilishinda mbele ya Borussia Dortmund katika Champions League wiki iliyopita bado alikuwa anawaheshimu wapinzani wake Chelsea kwenye mchezo wake wa nusu fainali ya Kombe la FA.

City jana ilikuwa anapambana na Kocha Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel ambaye yeye alikuwa amefanya mabadiliko kwa wachezaji wake watatu na alishuhudia timu yake ikishinda bao 1-0 mbele ya City kwa bao la Hakim Ziyech dakika ya 55 na kufanya Chelsea kutinga hatua ya fainali ya Kombe la FA.

Guardiola amesema:"Unadhani kwamba sikuweza kuweka nguvu kubwa kwenye mchezo wetu wa Kombe la FA? Unadhani kwamba Sterling ama Ferran Torres ama Gabriel Jesus hawastahili kucheza mchezo huu.

"Hatukuwa tumekata tamaa tulikuwa tunahitaji kufika kwenye fainali ya Kombe la FA ila tumepoteza. Kwa maana hiyo ikitokea umeshinda ina maanisha kwamba maamuzi yalikuwa mabaya?



"Rafiki yangu haipo hivyo haikuwa bahati yetu jambo ambalo limefanya tumeshindwa kupata ushindi. Timu ambayo imetinga hatua ya nusu fainali huwezi kuibeza labda useme kwamba tumepoteza mchezo hilo lipo wazi.

"Ulikuwa ni mchezo mgumu ninawapongeza wapinzani wetu Chelsea kwa ushindi. Licha ya kuwa na mabadiliko ya wachezaji hawa nane unadhani kama ingetokea tukashinda hapo mambo yangekuwaje? "

1 COMMENTS:

  1. Kapigwa tuu na alizidiwa,mambo mengine ni kelele tuu atulize asonge mbele

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic