April 18, 2021


 MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Ali Kiba jana alifanikiwa kutimiza majukumu yake kwa umakini na kuifanya timu yake kushinda bao 1-0.

Kiba ambaye pia ni mchezaji wa mpira ni nahodha wa timu ya Bin Slum FC ambayo inashiriki Ramadhan Cup inayoendelea kila siku usiku, viwanja vya JK.

Wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya Asas Rangers Kiba ni yeye ambaye alipachika bao la ushindi kwa kichwa ndai ya 18 dk 27.

Mchezo mwingine ambao ulichezwa jana ulikuwa ni ule kati ya Silent Ocean ambao walishinda mabao 2-0 mbele  Scaba Scuba.

Kiba amesema:"Ninafurahi kuona kwamba nimefunga kwani kipaji kipo na uwezo tunao wa kufanya vizuri,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic