April 14, 2021


 HATUA za makundi tayari zimekamilika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na timu nane ambazo ni bora kwa Afrika zimetinga hatua ya robo fainali.

Shirikisho la Soka Africa, (Caf) linatarajia kucheza droo Aprili 30 na timu zikajua wapinzani wao katika kusaka bingwa mpya wa Afrika.

Kwa sasa bingwa mtetezi ni Al Ahly abaye alikuwa kundi moja na Klabu ya Simba kutoka Tanzania inayonolewa na Didier Gomes raia wa Ufaransa.

Hizi hapa klabu nane zilizofuzu hatua ya robo ni Simba, Al Ahly kutoka kundi A, Mamelodi Sundowns na CR Belouizdad kutoka kundi B, Wydad AC na  Kaizer Chiefs kutoka kundi C na Esperance na MC Alger kutoka kundi D.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic