IMEELEZWA kuwa mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alikuwa kocha mkuu wa Yanga anatarajiwa kuja Bongo muda wowote kuanzia sasa ili kupata muda wa kuwatambua wachezaji wake.
Kaze alifutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo jambo lililofanya afungashiwe virago jumlajumla.
Kwenye mzunguko wa pili Kaze alianza kwa kusuasua ambapo kwenye mechi sita, alishinda mechi moja mbele ya Mtibwa Sugar na alipoteza mchezo mmoja na ubao ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga huku akiwa na sare nne.
Kwa sasa Yanga ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ambaye mchezo wake wa kwanza alishuhudia ubao ukisoma Yanga 1-1 KMC.
Kocha ambaye anapewa nafasi ya kuja Bongo ni Sebastian Migne ili aje kurithi mikoba ya Kaze.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mchakato wa kumsaka kocha unaendelea na kila kitu kikiwa sawa kitawekwa wazi.
Mnajiandikia tu, kila siku habari ni hiyo hiyo
ReplyDelete