April 13, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hana mashaka na timu ambayo atakutana nayo hatua ya robo fainali kwa kuwa wachezaji wake wamekuwa bora kila wakati.

Ikiwa ni namba moja kwenye kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika imekusanya pointi 13 baada ya kucheza mechi sita ni miongoni mwa timu bora nane Afrika.

Gomes amesema kuwa anatambua kutakuwa na ushindani mkubwa ila ni wakati wa kuonyesha kwamba Simba ni timu kubwa Afrika kwa vitendo.

"Hatuna mashaka na timu ambayo tutakutana nayo kwenye hatua ya robo fainali, kila timu nina amini kwamba ni bora ila nasi pia lazima tuonyeshe kwamba tupo imara na tunaweza.

"Kwa sasa Simba ni miongoni mwa timu nane bora Afrika hapo lazima tufanye kweli kuonyesha ukubwa wetu na kuendelea kuwa bora," amesema.

Kwenye kundi A ni AS Vita ambayo ina pointi 7 na Al Merrikh yenye pointi mbili zimeishia hatua ya makundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic