MABOSI wa Azam FC wamejigamba kwamba jambo ambalo walikuwa wamelipanga mwanzoni mwa msimu bado wana ndoto za kulifikia wakati huu ambao wana mwendo wa ushindi kwenye Ligi Kuu Bara.
Azam ambao wanafundishwa na kocha Mzambia, George Lwandamina wapo kwenye mbio za ubingwa ambapo kwa sasa wana pointi 50 zikiwa 7 nyuma ya Yanga wenye 57 walio kileleni.
Msemaji wa Azam FC, Thabith Zakaria, amesema, kwamba wana matumaini ya kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo kutokana na kupata pointi muhimu katika michezo ambayo wanacheza.
“Tumefikisha pointi 50 na inatupa matumaini ya kufanya vizuri huko mbele tunapoenda, ni kitu kizuri kwetu, pointi hizi ni muhimu kwetu jambo letu tulilosema mwanzo wa msimu matumaini yanaendelea kuwepo na mwisho wa msimu tutajua nini kitakuwa mkononi lakini tunavyoenda mambo yatakuwa mazuri.”
Azam FC kwa kesho ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji mchezo utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.
Mungu awatangulie
ReplyDeleteBig up
ReplyDelete