April 7, 2021


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amemlaumu mwamuzi wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali ya kwanza, Felix Brych kwa kile alichodai kwamba alifanya maamuzi yake binafsi mbele ya nyota wake Sadio Mane.

Klopp alionekana akiwa hana furaha baada ya mchezaji wake Mane kuchezewa faulo kwenye eneo la penalti na nyota wa Madrid, Lucas Vazquez ila mwamuzi huyo raia wa Ujerumani alipeta bila kuwapa penalti Liverpool.

Kwa kupoteza robo fainali ya kwanza kunaongeza kazi kubwa ya kufanya kwa Liverpool ili kuweza kufufua matumaini ya kushinda  taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa ilikubali kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Real Madrid.

Mabao ya Real Madrid usiku wa kuamkia leo yalipachikwa na Vinicius Junior aliyepachika mabao mawili dakika ya 27 na 65 na bao moja alipachika Marco Asensio dakika ya 36. Bao pekee la Liverpool lilipachikwa na Mohamed Salah dakika ya 51 ilikuwa ni Uwanja wa Estadio Alfredo Di Stefano.

Klopp amesema:"Hali ilivyokuwa kwa Mane mimi sijui nini aliweza kuamua kwa kweli, nilimwambia baada ya mchezo kwamba sawa tumepoteza lakini kazi yako wewe ilikuwa ni kuchezesha mpira na kufanya yote yanayotakiwa.

"Bado kuhusu mchezo ninaweza kusema kwamba kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri hivyo ikiwa tunahitaji kusonga mbele hatua ya nusu fainali ni lazima tuanze vizuri kwenye mchezo wetu kipindi cha kwanza," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic