February 10, 2017Baadhi ya maofisa kutoka klabu ya Yanga na ofisini kwa Mwenyekiti wao Yanga, Yusuf Manji walilazimika kubaki katika kituo cha kati hadi usiku wa manane kwa kuwa hawakuwa wakijua Manji alikuwa amepelekwa wapi.


Lakini baadaye alirejeshwa katika kituo hicho Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, takribani saa sita usiku.


Baada ya Manji kurejeshwa na kuingizwa kituoni hapo, taratibu maofisa hao walianza kuondoka katika eneo hilo.

Kabla waliendelea kubaki hapo wakieleza walitaka kujua alipokuwa amelekwa.


Manji pamoja an na Mchungaji Josephat Gwajima walipakiwa kwenye gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser lenye rangi nyeupe, ilikuwa kama saa 10 na nusu jioni.Gari hilo lenya usajili namba T 213 ARS liliondoka kituoni hapo kuelekea Posta ya zamani na haijajulikana hadi sasa walipelekwa wapi na hawakuwa wamrejeshwa kituoni hapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV