KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Saido
Ntibazonkiza amepewa jukumu zito na kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi kwa
kuhakikisha anapambana na wachezaji wenzake kuisaidia timu hiyo kuchukua
ubingwa msimu huu.
Mwambusi
leo Jumamosi ataiongoza Yanga
katika mchezo wake wa kwanza akiwa kaimu kocha mkuu dhidi ya KMC ya
katika mchezo unaotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamini mkapa huku ukiwa ni mchezo wake wa kwanza
baada kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Cedric Kaze.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani timu hiyo zinasema kuwa kiungo huyo ni mmoja
ya kati ya wachezaji waliopewa majukumu makubwa na kocha huyo kwa kuhakikisha
wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa msimu licha ya kupinzani mkali kutoka kwa Simba.
“Mikakati imekuwa mingi sana kwa kuwa timu
inataka kupata ubingwa na ndiyo limekuwa lengo kubwa kwa sasa maana wapo
wachezaji waliotakiwa wabadilike na wapo waliopewa majukumu kutokana na uzoefu
wao.
“Sasa mtu Ntibazonkiza kocha ametaka
kwanza kujitoa na kuendelea kuwa kiongozi ndani na nje ya uwanja kutokana na
uzoefu wake lakini kuhakikisha Yanga
inapata matokeo zaidi katika kila mchezo ambao itacheza.” Amesema mtoa taarifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment