KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo kimewasili Tanzania kikitokea nchini Misri.
Simba ilikuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, nchini Misri na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Licha ya kupoteza mchezo huo wametinga hatua ya robo fainali na pointi zao ni 13 na Al Ahly ina pointi 11.
Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ni furaha kwao kurudi salama na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment