HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kikubwa kinachomfanya asifikirie kurejea Bongo ni kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi.
Thiery amesema kuwa kwa sasa yupo Rwanda akiendelea kufanya mambo yake ikiwa mambo yatakwenda sawa anaweza kufikiria kurudi Tanzania.
Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Msaidizi, Vincent Barnaba ambaye jana aliongoza kikosi hicho mbele ya Azam FC.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, ubao ulisoma Azam FC 2-0 Mtibwa Sugar na mabao yote yalifungwa na Prince Dube.
Thiery amesema:"Nipo Rwanda na sifikirii kurudi Tanzania kwani hatukuwa na maelewano mazuri na baadhi ya viongozi hayakuwa vizuri na hata viongozi wenyewe walikuwa wanajua,".
0 COMMENTS:
Post a Comment