April 10, 2021

 


CLATOUS Chota Chama wanapenda kumuita Mwamba wa Lusaka ama triple c ndani ya kikosi cha Simba amesema kuwa  bado kazi inaendelea katika Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Jana Aprili 9, Simba ilikwama kulinda rekodi yake ya kucheza mechi sita bila kufungwa baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly. 

Awali ilikuwa imecheza mechi tano, ilishinda nne na kulazimisha sare moja ilikuwa mbele ya Al Merrikh.


Licha ya kupoteza mchezo huo Simba inaongoza kundi A ikiwa na pointi 13 huku Al Ahly ikiwa nafasi ya pili na pointi 11.


Nyota huyo ambaye kwenye hatua za makundi amecheza jumla ya mechi 6 na kutupia mabao mawili na pasi tatu amesema kuwa kazi bado inaendelea.


Kiungo huyo chaguo la Kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema:-"Tulikuwa na mchezo mzuri jana dhidi ya wapinzani wetu ambao ni imara katika bara hili.


"Nina amini kwamba tutaonana kwenye hatua ya robo fainali kwa kuwa mchezo ndo kwanza unaanza,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic