April 22, 2021


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa huwa anapata tabu kupanga kikosi chake pale ambapo mshambuliaji wake Karim Benzema anakuwa hayupo katika mpango wa mchezo wake.

Mshambuliaji huyo alijiunga na kikosi cha Real Madrid msimu wa 2014 rekodi zinaonyesha kwamba hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu katika michuano yote akiwa ndani ya timu hiyo.

Zidane amesema kuwa nyota huyo amekuwa akionyesha kiwango bora muda wote jambo ambalo ni bora kwake na timu pia.

"Benzema amekuwa akionyesha kiwango cha juu sana uwanjani  lakini kila mara amekuwa akiwaongoza wenzake kufanya kazi kutokana na uzoefu wake mkubwa.

"Huyu ni mmoja kati ya wachezaji ambao ni wakongwe kwenye soka, ukitazama hata maamuzi yake kwenye kila mchezo yamekuwa sahihi.

"Nimekuwa nikipata wakati mgumu  uwanjani kila ninapomkosa uwanjani," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic