April 22, 2021


KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier 
Gomes Da Rosa, ameweka wazi kuwa hawatakuwa tayari kuona wanashindwa kutwaa ubingwa mbele ya wapinzani wao Yanga kwa kuwa wana kikosi bora kilichofanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gomes ana kibarua cha kupambania kutetea taji la ligi ambalo Simba ilitwaa msimu uliopita wa 2019/20 huku watani zao wa jadi Yanga nao wakiweka wazi kwamba wanalihitaji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gomes amesema kuwa mipango yao kwa sasa ipo katika mechi zao za ligi kwa kuwa wamedhamiria kutetea ubingwa wao bila ya kujali anayeongoza ligi hiyo kwa sasa ni nani.

“Kitu kikubwa ambacho tunakiangalia katika ligi ni kuhakikisha tunapata matokeo bora katika kila mchezo bila ya kujali tunacheza na timu gani, kwa sababu malengo yetu ni kuweza kutetea ubingwa, jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu.

 "Kulingana na matokeo makubwa ambayo tunayapata kwenye mechi ambazo tunacheza inatupa nafasi ya kuamini kwamba itakuwa hivyo.


“Unajua hatuwezi kuwa na presha kwa kuwa wao wanaongoza ligi, sisi tunachokiangalia kwa sasa ni kushinda kila mchezo kutokana na mikakati yetu kulingana na mechi husika, naamini jambo la ubingwa kwetu lipo ndani ya uwezo wetu na linawezekana kwa asilimia zote kwa sababu Simba ina ubora mkubwa katika soka la Afrika kwa sasa, " amesema Gomes.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili ina pointi 55 baada ya kucheza mechi 23,vinara ni Yanga wenye pointi 57 baada ya kucheza mechi 26.

1 COMMENTS:

  1. Ushindi wa Mnyama kesho itaishusha Yanga kileleni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic