April 21, 2021



RASMI European Super League Cup imesimamishwa baada ya timu zote ambazo zilikubali kushiriki ligi hiyo mpya kujitoa jumlajumla kutokana na shinikizo kutoka kwa mashabiki kupinga ligi hiyo pamoja na Uefa kuigomea kabisa.

Mashabiki wengi walikuwa wanaigomea ligi hiyo mpya ambayo ilikuwa inahusisha timu zenye uwezo mkubwa kifedha na tayari timu 15 zilikuwa zimekubali kushiriki ligi hiyo iliyokuwa inapingana na Uefa pamoja na Fifa.

Miongoni mwa mashabiki ambao walijitokeza kupinga ligi hiyo ni pamoja na wale wa Chelsea ambao kabla ya mchezo  wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Stamford Bridge dhidi ya Brighton na kukamilika kwa sare ya bila kufungana walikuwa wakiishinikiza timu hiyo ijitoe kwa kuwa ilikuwa ni miongoni mwa timu ambazo zilikubali kushiriki ligi hiyo mpya.

Timu kubwa ambazo zilikubali kushiriki ligi hiyo ambayo ilianza fukuto Aprili 18,2021 na kuzimwa Aprili 20, ikiwa ni pamoja na Manchester United, Liverpool, Arsenal, Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid na Tottenham nazo pia zilithibitisha kujitoa kwenye ligi hiyo ambayo Shirikisho la Soka la Ulaya, Uefa liliweka wazi kuwa wote ambao watashiriki michuano hiyo mipya watafungiwa haraka sana.



4 COMMENTS:

  1. Nadhani Mh Salehe ukiwa Mwandishi Mwandamizi wa michezo unayejua soka hususan utanisaidia kwenye hili cse wawekezaji na Wana siasa lao moja always kupata kila fursa iliyopo mbele yao,Kama unaweza kujikita kwenye uwekezaji na Biashara utaweza kujua gharama yake kwamba utatazama kila fursa uitumie,Kwa fikra zangu niliwahi kuhoji Uwekezaji kwenye soka la Uingereza ,
    mimi huwa, pale nasema Ile ni siasa ya kuendelea kutukamata mawazo hasa kwa Yale Mataifa makubwa (Marekani,Russia,China)hao wengine ni mawakala wao ila Wanatumika kutuzuga eg wale mabosi wa Man City nk.Hapa tunaona Siasa za kutawala Dunia zinapo kamata watu,Tukubali Mwanadamu ni kitu gani mbele ya Mungu?Hawa jamaa wanatafuta pesa na himaya kwa nguvu ,wanatumia kila njia iliyopo kupata pesa,bila kujali hasara .Leo Wazungu wangekuwa na akili za Kiswahili Kama sisi (weusi Waafrika) hiyo Ligi ingechezwa,tu cse mngetumika ninyi waandishi kuhamasisha,Kama ilivyo hapa Tz Uwekezaji wa AZAM na Mo Sasa ndiyo wanaelekeza ratiba ya Ligi iendeje ,kwamba hii mechi ondoa ngumu kwetu na Ile sogeza pale, kisa tunacheza CAF club competitions

    ReplyDelete
  2. Ok Fala Mimi mpaka awekezwe aliye kuzaa ndipo utajua

    ReplyDelete
  3. Upo sahihi Ila Kwa mtazamo wako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic