April 13, 2021


 MABOSI wa Arsenal wameweka wazi kuwa bei ya nyota wao Lucas Torreira haiwezi kuwa chini ya pauni milioni 15 ikiwa kuna timu itahitaji huduma yake.

Kiungo huyo kwa sasa ameonyesha nia ya kuibuka ndani ya kikosi cha Boca Juniors ili apate changamoto mpya na hana mpango wa kurejea ndani ya Uwanja wa Emirates.

Kiungo huyo amepelekwa kwa mkopo Atletico Madrid na yupo hapo kwa muda tangu mwanzoni mwa msimu huu ila mambo kwake bado ni magumu.

Pia alimpoteza mama yake hivi karibuni baada ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona jambo ambalo linazidi kumfanya awe katika kipindi kigumu kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta ambaye amesema kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa karibu na mama yake.

 Alinunuliwa na Arsenal kutoka Klabu ya Sampdoria kwa pauni milioni 26 miaka mitatu iliyopita na sasa wapo tayari kumuachia kuanzia pauni milioni 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic