KLABU ya Yanga inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ghafla mwendo wake umebadilika mzunguko wa pili kutokana na kupata matokeo ya kususua tofauti na awali ilipoanza ligi.
Yanga mzunguko wa kwanza iliweza kuwa na kasi ambapo kwenye mechi zake tano za mwanzo ilizocheza iliweza kushinda mechi nne na kulazimisha sare moja zama zile za Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na uwezo wa kukinoa kikosi hicho.
Nafasi yake ilichukuliwa na Cedric Kaze ambaye aliongoza kikosi kwenye jumla ya mechi 18 ambapo alipoteza mchezo mmoja, sare 7 na alishinda mechi 10 alifutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovo wa timu yake.
Kaze alisema kuwa anafurahi kupata nafasi ya kuwa mwalimu kwenye timu hiyo huku akijivunia kuwapa taji la Mapinduzi baada ya kushinda mbele ya Simba kwenye fainali kwa penalti.
Mzunguko wa pili Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi saba imelazimisha sare tano, imeshinda mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.
Ilikuwa mbele ya Coastal Union ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ambapo ulikuwa ni mchezo wa kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 kwa Yanga kupoteza.
Ushindi wake ulikuwa mbele ya Mtibwa Sugar na ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.
Sare za Yanga zilikuwa namna hii:-Mbeya City 1-1 Yanga, Tanzania Prisons 1-1 Yanga, Polisi Tanzania 1-1 Yanga na Yanga 1-1 KMC.
Imefunga jumla ya mabao 9 safu yake ya ushambuliaji kwenye mechi 7 na imeruhusu jumla ya mabao 9 safu yake ya ulinzi.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza jumla ya mechi 24 na pointi zake ni 51.
0 COMMENTS:
Post a Comment