April 18, 2021


 IMEELEZWA kuwa Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya Kayky da Silva.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 anakipiga ndani ya Klabu ya Fluminense ni raia wa Brazil.

Mpango huo ambao umezidi kupamba moto ni sawa na ule ambao waliweza kuufanikisha kwa kuinasa saini ya Gabriel Jesus, 2017 na walimsajili akiwa na miaka 19 akitokea Klabu ya Palmeiras.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari kutoka Italia, Fabrizio Roman amesema kuwa City imekubali kutoa Euro milioni 10 kama ada ya uhamisho pamoja na asilimia 20 ya mauzo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic