April 29, 2021


KOCHA wa makipa wa kikosi cha Yanga, Razack Siwa amesema kuwa walivurugwa baada ya kufungwa bao na Prince Dube kwa kuwa liliharibu mipango yao ya kusaka pointi tatu.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ilikubali kuyeyusha pointi tatu mazima mbele ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 25.

Ni Dube ambaye alipachika bao hilo dakika ya 85 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 baada ya mpira uliopigwa na mkongwe Agrey Morris kumgonga beki Abdalah Shaibu, ‘Ninja’.

Akizungumza na Saleh Jembe, Siwa amesema kuwa walijipanga kupata pointi tatu ila baada ya kufungwa na Dube bao hilo lilivuruga mipango yao.

“Tulikuwa tunahitaji kupata pointi tatu ila baada ya kufungwa lile bao lilivuruga mipango yetu. Ilikuwa ni targeti ya mchezaji, kipa yoyote anaweza kufungwa bao lile hasa ukizingatia kwamba mshambuliaji alikuwa anafikiria na anajua kile ambacho anakihitaji.

“Pigo lake lilikuwa sahihi na kwa wakati sahihi hivyo hakuna wa kumlaumu, bado tuna mechi nyingine za kufanya tunajipanga na tutafanya vizuri,” amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili na pointi zake ni 57 baada ya kucheza mechi 27, Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 54 baada ya kucheza mechi 27 na kinara ni Simba mwenye pointi 61 baada ya kucheza mechi 25.

3 COMMENTS:

  1. Hii mechi ilishapita nyinyi mbona mnatuletea historia hamna habari nyingine za maana???

    ReplyDelete
  2. Kwani kuanzia dk ya kwanza Yanga walikuwa wapi kufunga? Mbona Siwa unatuchanganya?

    ReplyDelete
  3. Yanga katika mchezo mzima haikuwa bora kuliko Azam na kufungwa haikuwa jambo geni kama itavokuwa hiyo siku ya siku na Mnyama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic