UNAAMBIWA Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameamua kuichukulia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita kama fainali na kuna mzigo ambao umetengwa.
Taarifa
za ndani zinadai kuwa hadi kufikia sasa kuna mamilioni ya fedha yametumika na
mengine yatatumika ambapo jumla ni shilingi milioni 600 ili kuongeza motisha
kwa wachezaji na benchi la ufundi kama watafanikiwa kuvuna pointi tatu.
Leo, Simba inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es
Salaam, kuwakabili AS Vita Club ya DR Congo kwenye mchezo wa marudio ikiwa na
kumbukumbu ya kuvuna pointi tatu kwenye mechi ya kwanza ya ugenini.
Simba
ndiyo kinara wa Kundi A kwa kuwa na pointi 10, ilizozikusanya baada ya kucheza
dhidi ya AS Vita ugenini, Al Ahly ya Misri nyumbani, Al Merrikh ya Sudan
nyumbani na ugenini pia.
Habari zimeeleza kuwa tayari marafiki wa
Mo, ambao nao ni watu wenye fedha, wamekuwa wakichanga kila kunapokuwa na mechi
muhimu na wameshamuahidi katika mchezo huu kuwa watachangia katika fedha
atakazowapa benchi la ufundi na wachezaji.
“Kwa
ahadi ambayo nimeisikia kutoka kwa bosi wetu Mo, hadi sasa sina shaka juu ya
wachezaji wetu kuvuna pointi tatu mbele ya AS Vita, maana tajiri tayari
ameshaunganishiwa nguvu na marafiki zake.
“Bosi
hataki utani kabisa kwenye mchezo huo, kwani amesema ni bora watumie fedha nyingi
kutoa motisha kwa wachezaji ili washinde hapa nyumbani na siyo kusubiria kule
Misri ambako naamini kama tukikosa uhakika wa ushindi hapa itakuwa ngumu sana
kupata pointi tatu au moja tunayohitaji ili tusonge mbele,” kilisema chanzo
hicho.
Pambano hili muhimu sana, vita apigwe
ReplyDelete