April 3, 2021


USISHANGAE kuona mchezo ujao wa Yanga dhidi ya KMC safu yao ya ulinzi ikaongozwa na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Dickson Job baada ya kutajwa kuwa wamekuwa wakipewa kipaumbele mazoezini na kocha Juma Mwambusi.

 

Chanzo hicho makini kilidokeza kuwa tangu Job amepona majeraha na kurejea mazoezini amekuwa akifanya vizuri na mara zote amekuwa akipangwa na Ninja kwenye mazoezi, hata katika michezo ya kirafiki na ile ya timu za vijana wamekuwa wakicheza kwa kiwango cha juu.

 

Taarifa imeeleza: “Wakati Bakari Nondo akiwa timu ya taifa, Mwambusi alikuwa anawatumia Job na Ninja wakicheza kama mabeki wa kati, hiyo ni kwenye mazoezi na kwenye ile michezo ya kirafiki dhidi ya timu ya vijana ya U20. Inavyowezekana hata mechi ijayo huenda wao wakaanza.”

 

Alipotafutwa kocha Mwambusi simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa na alipotafutwa Job alikiri kuwa amekuwa akicheza pacha na Ninja kwenye mazoezi ya timu na hiyo ni tangu aliporejea kambini kutoka timu ya taifa.

 

“Kweli kwenye mazoezi nimekuwa nikicheza sana na Ninja, sasa sijajua mwalimu analenga kitu gani. Ingawa kwa upande wangu imenisaidia na nimekuwa fiti sasa kucheza mchezo wowote nikiwa na timu hii,” alisema Job.


Chanzo: Championi

1 COMMENTS:

  1. Ninatoa ushauri kutoka moyoni. Yanga watafute beki kisiki badala ya Mwamnyeto. Mwamnyeto anapitwa kirahisi sana na maadui na hana mbio. Mara nyingi mechi wanazopoteza Yanga asilimia kubwa zinatoka kwa Mwamnyeto.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic