MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdoul Razack ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, tayari ameanza mazungumzo na klabu tatu tofauti ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji saini yake.
Fiston aliyejiunga na Yanga Januari, mwaka huu, mkataba wake na Yanga umebaki takribani miezi miwili kabla ya kumalizika.
Nyota huyo raia wa Burundi baada ya kujiunga na Yanga bado hajaonyesha makeke yake kwenye kikosi hicho tofauti na wengi walivyokuwa wakifikiria.
Ametupia bao moja kwenye ligi kuu na FA moja. Timu yake ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 25.
Mrundi huyo amesema: “Kila mtu anaweza kuwa anajiuliza je, nimeongezewa mkataba au hatima yangu itakuwaje bila kutaka kujua je, ikinibidi kuongeza mkataba nipo tayari?
“Ndio, nipo kwenye mazungumzo na klabu zaidi ya tatu na tukifikia makubaliano mtazijua, pia sihitaji kuulizwa maswali kuhusu mkataba, ngoja niweke akili yangu kwenye mechi zilizobaki, bado tuna kazi ngumu ya kupigania ubingwa.”
Chanzo:Championi
0 COMMENTS:
Post a Comment