KINACHOFANYWA na Simba kwa sasa ni ishara ya kuwa timu hiyo imekuwa kwenye ubora wake wa hali ya juu mara baada ya kucheza kandanda safi na kuwa na uwezo wa kupiga pasi kuanzia nyuma hadi wanakwenda kufunga bao.
Katika michezo yote waliyocheza Uwanja wa Mkapa kuanzia ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mchezo wa Jumatano wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa, Simba walikuwa wana wastani wa kupiga pasi 15 wakiwa wanakwenda kushambulia bila timu pinzani kuugusa mpira.
Bao la kwanza la Simba lililofungwa na Clatous Chama dakika ya 9 ya mchezo, Simba walipiga pasi 16 kuanzia nyuma hadi wanaingia eneo la hatari la Mtibwa na Simba kupata ‘free kick’ iliyowekwa kambani na Chama.
Bao la pili lililofungwa na Larry Bwalya dakika ya 19 ya mchezo, Simba walipiga pasi 13 hadi kupatikana kwa goli hilo, mabao mawili ya Meddie Kagere dakika ya 43 na 52 Simba walipiga pasi 14 kwenye kila bao huku lile la tano la Luis Miquissone Simba walipiga pasi 11.
Wakati Simba wakitakata kwa namna hiyo, Mtibwa wenyewe walikuwa na wastani wa kupiga pasi tano tu.
Kocha wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, alionyesha kufurahishwa na kiwango cha timu yake na aliliambia kuwa:“Hakika nafurahishwa na uwezo na kiwango cha ujumla ambacho kinaonyeshwa na wachezaji wangu, bila shaka tupo kwenye ule ubora ambao tunastahili kuwa nao kwa sasa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment