LICHA ya kuwa na mwendo wa kobe kwenye kucheka na nyavu, mshambuliaji namba moja wa Yanga, Yacouba Songne mwenye mabao sita na pasi nne kati ya mabao 41 amepitishwa na makocha wa mataifa manne kwenye kikosi cha kwanza.
Yanga iliyo nafasi ya pili imeongozwa na makocha wanne mpaka
sasa kwa msimu wa 2020/21 kutoka mataifa manne tofauti, ambapo walianza msimu
na taifa la Serbia kisha Burundi,Tanzania na sasa ni Tunisia.
Amecheza jumla ya mechi 22 za ligi kati ya 27 ambazo Yanga
imecheza amekosekana kwenye mechi tano na kumfanya atumie jumla dakika 1,375.
Zama za Zlatko Krmpotic, kutoka Serbia alicheza mechi tano na
kutumia jumla ya dakika 253, ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, dk 45, Mbeya
City,dk 45, Kagera Sugar, dk 55, Mtibwa Sugar,dk 18, Coastal Union, dk 90.
Zama za Cedric Kaze raia wa Burundi, alitumia dakika 794 katika
mechi 13 alizocheza ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania, dk 63, KMC,dk 2, Biashara
United,dk 8, Gwambina FC, dk 82, Simba, dk 12, Azam FC, dk 90, JKT Tanzania, dk
54, Ruvu Shooting,dk 90. Mwadui,dk 66, Dodoma Jiji dk 89, Azam FC,dk 90,
Coastal Union,dk 58, Ihefu,dk 90,
Mbele ya Juma Mwambusi ambaye ni Mtanzania alicheza mechi tatu
na kutumia dakika 238 ilikuwa mbele ya KMC, dk 87, Biashara United,dk 83, na
mbele ya Gwambina, dk 68.
Mechi ya kwanza ya Nassredine Nabi raia wa Tunisia ndani ya
Yanga alianza kikosi cha kwanza mbele ya Azam FC na aliyeyusha dakika zote 90.
Kwa sasa yupo na kikosi cha Yanga ambacho kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora, kesho Aprili 30, Uwanja wa Nelson Mandela.
Upuzi mtupu yaani
ReplyDelete