April 14, 2021


 SOUD Slim, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa watakachoifanya leo Simba Uwanja wa Mkapa hawataamini baada ya dakika 90 kukamilika.

Mtibwa Sugar itakaribishwa na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na mipango ya timu zote mbili.

Mtibwa Sugar kwenye msimamo ipo nafasi ya 15 ikiwa imecheza jumla ya mechi 23  na ina pointi 24 ipo kwenye harakati za kujinasua kwenye kushuka daraja kutokana na mwendo wake wa kusuasua katika ligi.

Inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 20 na kujikusanyia pointi 46 ikiwa na hesabu za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Slim amesema kuwa wengi wanafikiria wapinzani wao watapata matokeo mazuri ila hilo halitawezekana kwa kuwa wamejipanga kuwashangaza.

"Ninajua kwamba wengi wanadhani tutapoteza mchezo wetu dhidi ya Simba ila hawataamini kile ambacho watakiona.

"Maandalizi yapo vizuri, makosa yetu kwenye mechi zilizopita tumeyafanyia kazi na tunaamini kwamba tutapata ushindi hakuna ambacho tunakihitaji kwa sasa.

"Ukitazama msimamo unaona kwamba hatupo kwenye nafasi nzuri ni lazima tupambane, wachezaji wapo tayari na benchi la ufundi limejipanga," amesema.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri ni Mzamiru Yassin alianza kuwafunga Mtibwa kisha Boban Zirintusa wa Mtibwa Sugar aliwaweka mzani sawa na kufanya ukuta kusoma Mtibwa Sugar 1-1 Simba.

3 COMMENTS:

  1. Mtakamia weeee baada ya hapo mnaendelea na mambo yenu ya kufungwa

    ReplyDelete
  2. Kuwa makini na maneno yako hayo we kocha. Tutakutafuta baada ya mechi tuone nani hataamini kitakachotokea

    ReplyDelete
  3. Wapi kocha wa Mtibwa...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic